• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serena, Federer na Nadal wafuzu robo fainali Wimbledon

  (GMT+08:00) 2018-07-10 10:10:50

  Wachezaji nguli wa mchezo wa tennis Serena Williams wa Marekani, Roger Federer wa Uswisi, na Rafael Nadal wa Hispania wamefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Wimbledon, baada ya ushindi waliopata kwenye mechi zao za jana.

  Serena alimshinda Evgeniya Rodina wa Urusi kwa seti ya 6-2, 6-2 na katika hatua ijayo atacheza na Giorgi wa Italia.

  Roger Federer amefuzu kwa kumshinda Adriana Mannarino wa Ufaransa, na kwenye mechi ya ijayo ataumana na Kevin Anderson wa Afrika Kusini aliyefuzu kwa kumshinda Gael Monfils wa Ufaransa.

  Naye Rafael Nadal, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 amefuzu hatua ya robo fainali, kwa kumfunga Jiri Veserly wa Jamhuri ya Czech.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako