• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya Madini Tanzania kujenga vituo saba wachimbaji

  (GMT+08:00) 2018-07-10 19:56:49
  Wizara ya Madini nchini Tanzania itatumia Sh bilioni 11.9 kujenga vituo saba vya umahiri na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Chuo cha Madini jijini Dodoma.

  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki ameelezea mkakati wa ujenzi huo baada ya kusaini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo hivyo na Suma JKT itakayojenga vituo hivyo kwa miezi sita tangu Julai hii hadi Desemba mwaka huu.

  Waziri Kairuki alisema kwa kuitumia Suma JKT badala ya mkandarasi mwingine, wizara itaokoa Sh milioni 249.3 ambazo zitaisaidia wizara katika kutekeleza majukumu mengine.

  Amesema vituo hivyo vitajengwa Mpanda, Songea, Chunya, Handeni, Bariadi, Bukoba na Musoma na vitatoa mafunzo ya jiolojia hasa utafiti wa madini, ya uchenjuaji madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hasa teknolojia zisizotumia kemikali ya zebaki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako