• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano kati ya China na Ulaya waingiza nishati kwa uchumi wa dunia

  (GMT+08:00) 2018-07-10 20:09:54

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alifanya ziara katika nchi za Bulgaria na Ujerumani kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 10 mwezi huu, ambapo alihudhuria mkutano wa 7 wa viongozi wa China na nchi za Ulaya ya kati na mashariki, na kuendesha duru ya 5 ya mazungumzo kati ya serikali za China na Ujerumani.

  Kuimarika kwa ushirikiano kati ya China na Ulaya kunasaidia kutimiza ushirikiano wa karibu kati ya pande hizo mbili, kunasaidia pande hizo mbili kusaidiana kiuchumi, na kutumia mazingira yenyewe ya kila upande, kuinua kiwango cha maisha ya watu. Chini ya hali ya sasa ya kuwa na wazo la upande mmoja, kujilinda kibiashara na upinzani wa utandawazi wa kichumi, ufuatiliaji na maslahi ya pamoja ya China na Ulaya umekuwa mkubwa zaidi, ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali utaingiza nguvu kwa uchumi wa dunia unaotishiwa na vita ya kibiashara.

  Hivi sasa, mikwaruzano inayosababishwa na kujilinda kibiashara na msimamo wa upande mmoja unaochochewa na Marekani inatokea mmoja baada ya mwingine, uonevu wa kibiashara wa Marekani umeathiri vibaya mfumo wa biashara huria ya dunia, na kanuni za kimataifa. Kama Marekani inaendelea kufanya hivyo, utulivu na ufufukaji wa uchumi wa dunia utaharibiwa. Katika kipindi hiki muhimu, China na Ulaya zinapaswa kushirikiana zaidi, kuunga mkono biashara huria na kurahisisha uwekezaji, na kulinda uchumi wa dunia wa kufungua mlango na mfumo wa biashara wenye ncha nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako