• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China na chansela wa Ujerumani wahudhuria maonesho ya magari yanayojiendesha

    (GMT+08:00) 2018-07-11 07:27:32

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel wamehudhuria maonesho ya magari yanayojiendesha ya China na Ujerumani.

    Bw. Li amesema, maonesho hayo ni shughuli muhimu katika ziara yake nchini Ujerumani. Katika miaka 40 iliyopita, kampuni za Ujerumani zimeonesha ujasiri na busara, na kuwa za kwanza kuanzisha ushirikiano na China kwenye sekta ya magari. Amesema magari yanayojiendesha yanawakilisha kiwango cha juu zaidi cha ufundi wa magari na yana mustakabali mzuri.

    Pia amesema, China itafungua zaidi soko la magari, na inakaribisha kampuni za Ujerumani kupanua uwekezaji nchini China, kuimarisha ushirikiano wa teknolojia ya juu, na kugeuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika utengenezaji wa magari, hadi kwenye utafiti na utafiti na utafiti na ubunifu wa akili bandia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako