• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtaalamu asema China inaweza kuziba pengo linalotokana na kupungua kwa uagizaji wa soya za Marekani katika soko la China

  (GMT+08:00) 2018-07-11 13:54:47

  Mchumi mwandamizi wa Kituo cha Habari cha Nafaka na Mafuta cha Taifa cha China Wang Liaowei, amesema vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya China iliyochukuliwa kama ni kubwa zaidi katika historia ya uchumi, itabadilisha muundo wa biashara wa soya duniani.

  Tarehe 6 Julai, Marekani ilianza kuongeza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 34 zinazoingia katika soko la Marekani, na China ililazimika kujibu kitendo hicho kwa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani zinazoingia kwenye soko la China ikiwemo soya. Marekani ni nchi ya pili inayouza soya kwa wingi zaidi nje ya nchi, na mwaka wa 2017 hadi 2018, soya ya Marekani iliyouzwa nje ya nchi imechukua asilimia 37 ya biashara ya soya duniani. China ni na inayoagiza soya kwa wingi zaidi kutoka nje ya nchi, na inaweza kuchukua asilimia 60 ya soya yote duniani.

  Mchumi mwandamizi wa Kituo cha Habari cha Nafaka na Mafuta cha Taifa cha China Wang Liaowei, amesema kutokana na kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, China kuongeza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya soya ya Marekani kutasababisha bei ya soya ya Marekani kukosa nguvu ya ushindani kwenye soko la China, na muundo wa biashara ya soya duniani utabadilika kabisa. Anasema, "Kama bei ya soya za Marekani ni kubwa kuliko ile ya Brazil, hakika kampuni za China zitapunguza kuagiza soya kutoka Marekani, badala yake, zitaangalia soya kutoka nchi za Amerika Kusini kama vile Brazil na Argentina, halafu mtirirko mzima wa bidhaa utabadilika na uwiano mpya wa biashara ya soya duniani utapatikana."

  China ni soko kubwa zaidi kwa soya ya Marekani, na mwaka jana, soya ya Marekani iliyouzwa nchini China ilichukua theluthi moja ya soya ya Marekani iliyouzwa nje ya nchi. Hivi karibuni, wasiwasi na mustakbali wa uuzaji soya nje ya Marekani umesababisha kupungua kwa bei ya soya, na kusababisha wakulima wa Marekani kupata hasara kubwa.

  Bw. Wang ameongeza kuwa athari zinazotokana na kupunguza kuagiza soya ya Marekani zitaanza kuonekana mwezi wa 10 hadi mwezi Februari mwakani, ambapo huenda China itaagiza soya ya Marekani kwa bei kubwa, lakini baada ya mwezi Machi mwakani, soya inayoagizwa kutoka nje ya China itakuwa ya kutosha. Na Inaaminika kuwa katika mwaka mmoja hadi miaka miwili ijayo, China inaweza kuziba pengo linalotokana na kuondolewa kwa soya kutoka Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako