• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya biashara ya China yatoa kauli kuhusu taarifa ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa nyingine za China

  (GMT+08:00) 2018-07-11 16:52:55

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Gao Feng amepinga vikali dhidi ya taarifa ya Marekani ya kutoa orodha ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 zitakazoongezewa ushuru.

  Amesema Marekani imetoa orodha ya bidhaa zitakazotozwa ushuru kwa njia isiyo sahihi, na hili halikubaliki na China inapinga vikali hatua hiyo. Ameongeza kuwa, kwa kufanya hivyo, Marekani inaiumiza China, dunia, na kuumia yenyewe, na kwamba kitendo hiki kinakwenda kinyume na maslahi ya watu.

  Msemaji huyo amesema China itawasilisha mara moja malalamiko ya ziada kwa Shirika la Biashara Duniani WTO juu ya vitendo vya upande mmoja vya Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako