• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Taasisi za serilai kuungwa katika mfumo wa ununuzi wa serikali

    (GMT+08:00) 2018-07-11 20:43:35
    Waziri wa Fedha na Mipango ,Dk Philip Mpango ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ,kuhakikisha taasisi zote za serikali zinajiunga na Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya mtandao (TANePS),ili kudhibiti na kuondoa urasimu uliokuwa ukifanyika kwenye manunuzi.

    Dk mpango alitoa agizo hilo jana alipotembelea banda la PPRA lililopo kwenye Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara.

    Pia aliitaka PPRA kuweka muda wa mwisho wa taasisi hizo kujiunga na mfumo huo na kuwataka wazichukulie hatua zile ambazo hazitakuwa zimejiunga katika kipindi watakachoweka.

    Alisema ni lazima taasisi zote zinazoanzishwa ambazo zina ununuzi mkubwa kujiunga na mfumo huo.

    Alisema serikali inaibiwa fedha nyingi kwenye ununuzi wa umma ,hivyo ni wajibu wa PPRA kuzibana taasisi hizo.

    Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Umma PPRA,Bertha Soka,alisema tayari mfumo huo umeshaanza kufanya kazi kwa kuziunga taasisi 100 za umma zinazohusika na ununuzi wa vifaa tiba na dawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako