• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa NATO waanza kwa mivutano kati ya wanachama

  (GMT+08:00) 2018-07-12 08:44:40

  Mkutano wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO umeanza mjini Brussels huku kukiwa na kurushiana maneno, baada ya Rais wa Marekani kuweka wazi kuhusu mvutano kuhusu uchangiaji wa gharama na ushawishi nje ya NATO.

  Katika siku ya kwanza ya mkutano Rais Donald Trump wa Marekani alizusha tafrani baada ya kusema Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel kuwa anayumbishwa na maslahi ya Russia. Bw. Trump alisema Ujerumani inadhibitiwa kabisa na Russia kwa kuwa inapata asilimia 60 hadi 70 ya nishati yake kutoka kwa Russia, na kusema utegemezi wa nishati kwa Russia "haufai". Rais Trump pia alisema Marekani inatoa asilimia 4.5 ya pato lake kwa NATO, wakati Ujerumani inatoa asilimia 1 tu.

  Muda mfupi baadaye Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel alisema Ujerumani ni mchangiaji mkubwa wa pili wa askari kwenye NATO na inashiriki vilivyo kwenye shughuli za NATO nchini Afghanistan, na kwa kufanya hivyo pia inalinda maslahi ya Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako