• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Kenya yawasaka wapiganaji wa kundi la al-Shabaab baada ya shambulizi dhidi ya kambikambi yao kushambuliwa

    (GMT+08:00) 2018-07-12 09:03:39

    Maofisa usalama wa Kenya wameanzisha msako dhidi ya wapiganaji wa kundi la al-Shabaab walioishambulia kambi ya polisi katika kaunti ya kaskazini mashariki ya Garissa, karibu na mpaka wa Somalia siku ya Jumanne Jumanne, na kuwajeruhi maofisa watatu wa polisi.

    Mratibu wa eneo la kaskazini mashariki Mohamud Saleh amesema kuwa washambuliaji hao waliodhaniwa kuvuka mpaka kutoka nchi jirani ya Somalia kwanza waliharibu mlingoti wa mawasiliano ya Safaricom kwa kutupa mabomu, na baadaye kuishambulia kambi ya polisi. Ameongeza kuwa vikosi vya usalama vimeimarisha doria katika mpaka na Somalia kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi katika maeneo hayo. Hili ni tukio jipya kama hili kutokea katika eneo hilo na mpaka sasa hakuna watu waliokamatwa.

    Habari pianyingine zinasema Kenya na Marekani zimetoa wito wa kufanywa kwa juhudi zaidi ili kutuliza hali ya Somalia na Sudan Kusini. Wito huo umetolewa baada ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kukutana na kamanda Mkuu wa uongozi waKamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika AFRICOM Bw. Thomas Waldhauser mjini Nairobi wakirudia ahadi zao za kutafuta amani katika nchi hizi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako