• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: CECAFA yaiongezea michuano Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-07-12 09:55:19

  Baraza la soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahidi kushirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), katika kufanikisha michuano ya kanda ya kuwania kufuzu fainali za AFCON kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, itakayoanza Agosti 11 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es salaam.

  Akizungumzia maandalizi kuelekea katika michuano hiyo itakayotumia uwanja wa Taifa na Chamazi, Katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye amesema, anaamini Tanzania itajitangaza vizuri kimataifa kupitia uandaaji wa mashindano makubwa ya soka ndani ya mwaka huu kama ilivyoanza na Kombe la Kagame.

  Michuano hiyo itashirikisha mataifa 10 na yamepangwa katika makundi mawili. Kundi A zimepangwa timu za Rwanda, Burundi, Somalia, Sudan na mwenyeji Tanzania huku kundi B likiwa na timu za Uganda, Kenya, Ethiopia, Sudani Kusini na Djibouti. Tanzania itafungua michuano hiyo Agosti 11 ikicheza dhidi ya Burundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako