• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kukidhi mahitaji ya soya kwa kuiagiza kutoka nchi nyingine

  (GMT+08:00) 2018-07-12 17:01:12

  China ni nchi ya kwanza kwa kuagiza ya soya, huku Marekani ikiwa nchi ya pili kwa kuuza bidhaa hiyo duniani. Vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani italeta athari kubwa kwa soko la soya duniani. Wataalamu na maofisa ya mashirika ya China wamesema, baada ya kuongezwa ushuru wa forodha, soya ya Marekani itakosa uwezo wa ushindani nchini China, na China itakidhi mahitaji ya soya kwa manunuzi kutoka nchi nyingine.

  Mwaka jana na mwaka huu, mauzo ya soya ya Marekani yanachukua asilimia 37 ya mauzo hayo yote duniani, huku manunuzi ya bidhaa hiyo ya China yakichukua asilimia 60 ya manunuzi hayo yote duniani. Mtaalamu wa idara ya habari za nafaka ya China Bw. Wang Liaowei amesema, baada ya kuongeza ushuru wa forodha kwa soya ya Marekani kwa asilimia 25, bei yake nchini China itakuwa ghali, na hali ambayo itasababisha mabadiliko makubwa kwa soko la soya duniani. Anasema,

  "Mashirika ya China yamepunguza kuagiza ya soya kutoka Marekani kuanzia mwezi Juni hatua kwa hatua. Kama bei ya soya ya Marekani ni juu kuliko soya ya Brazil, bila shaka China itainunua kutoka Brazil, na uwiano wa biashara ya soya duniani utajengwa upya."

  Madhumuni ya China ya kununua soya ni kutengeneza mafuta ya kula na chakula cha mifugo. Mkuu wa Shirika la nafaka la China Bw. Yu Xubo amesema, mafuta ya kula na chakula cha mifugo yanaweza kutengenezwa kwa vitu vingine vingi vinavyopatikana kwa rahisi kwenye soko la dunia. Anasema,

  "Kwa mfano mafuta ya kula, biashara ya bidhaa hiyo ni zaidi ya tani milioni 80 kwa mwaka duniani. Mahitaji ya mafuta ya soya pia yanaweza kukidhiwa kwa mafuta ya maharagwe mengine. Vilevile mahitaji ya chakula cha mifugo nchini China pia yanaweza kutoshelezwa kwa njia nyingine nyingi."

  Aidha, wataalamu wa nafaka wamesema China pia inaweza kukidhi mahitaji ya soya kwa njia ya kuongeza uzalishaji wa ndani, na kununua kutoka nchi nyingine. Wanaamini kuwa China itaondoa pengo la utoaji wa soya ndani ya mwaka mmoja au miwili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako