• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Serikali ya Uganda kuangalia upya kodi ya mitandao

  (GMT+08:00) 2018-07-12 19:27:34
  Serikali ya Uganda imesema itajadili upya kodi ya mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma pesa kwa simu.

  Kwa sasa serikali inatoza kodi ya shilingi 200 za Uganda sawa na dola 0.05 ili mtu aweze kutumia mitandao kama Twitter na Facebook.

  Watu wamekuwa wakiandamana kupinga kodi hoyo lakini bado hakuna hakikisho kuwa itaondolewa na huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya kuidhinishwa mageuzi.

  Bunge liliidhinisha kodi hiyo mnamo mwezi Mei baada ya rais Yoweri Museveni kushinikiza mageuzi hayo.

  Waziri wa habari na mawasiliano wa Uganda Frank Tumwebaze pia ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako