• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Ndege mpya ya Tanzania kuanza safari baad aya wiki tatu

  (GMT+08:00) 2018-07-12 19:27:38

  Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyowasili nchini Tanzania Jumapili iliyopita na kupokewa na Rais John Magufuli, itaanza safari zake za ndani baada ya wiki tatu.

  Ndege hiyo ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 262, itaanza kazi kwa kufanya safari za ndani ya nchi kwa takribani mwezi mmoja kabla ya kuanza safari za nje ya nchi.

  Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), Ladislaus Matindi, amesema sababu ya ndege hiyo kuanza kazi baada ya wiki tatu kuanzia sasa inatokana na matakwa ya kiusalama.

  Matindi aliyataja baadhi ya matakwa hayo ya kiusalama ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwanza kabla ya ndege hiyo kufanya safari za ndani na nje ya nchi ni pamoja na kutoa mafunzo ya uokoaji kwa wahusika watakaofanya kazi kwenye ndege hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako