• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifurushi zaidi ya bilioni 22 vyasambazwa nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-12 19:40:04

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa soko katika kituo cha utafiti wa maendeleo cha idara ya posta ya China Bibi Geng Yan leo hapa Beijing amesema, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China imesambaza vifurushi zaidi ya bilioni 22.

    Bi. Geng amesema, mtandao wa usambazaji wa vifurushi vya kimataifa umekamilika hatua kwa hatua, na shughuli za usambazaji wa vifurushi vya kimataifa zimekuwa sehemu muhimu ya ongezeko la sekta hiyo. Pia amesema, thamani ya uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa vifurushi imezidi dola bilioni 454 za kimarekani, ambayo ni ongezeko la asilimia 30 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Idadi hiyo imechukua asilimia 17 ya thamani ya jumla ya uuzaji bidhaa za rejareja kote duniani, na imekuwa njia muhimu ya mzunguko wa bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako