• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yapanga kutumia raslimali za bahari kuhimiza ongezeko la uchumi na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:13:28

  Serikali ya Kenya inapanga kutumia vizuri raslimali za baharini ili kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na mwitikio wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Monica Juma amesema msingi imara wa kisheria na sera unaboreshwa, ili kuhimiza ongezeko la uchumi kutokana na sekta ya mambo ya bahari na kufanya liendane na ajenda ya Big Four ya Rais Uhuru Kenyatta.

  Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano kuhusu usalama baharini nchini Somalia na kwenye nchi za magharibi mwa Pwani ya bahari ya Hindi, Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Monica Juma, amesema kwa sasa wanatafuta njia zenye ubunifu za kusimamia bahari na kuanzisha na mipango ya maendeleo ya taifa na mipango ya kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa.

  Wajumbe 200 kutoka nchi 69 wamehudhuria mkutano huo, wakiwa ni pamoja na mawaziri, na wataalam wa usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako