• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa watoa dola za kimarekani milioni 15 kuwasaidia watu waliopoteza makazi nchini Ethiopia

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:51:07

  Mfuko wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kuongeza msaada wa kibinadamu kwa watu walioathirika na mgogoro unaopamba moto kati ya jamii tofauti nchini Ethiopia.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema wakati hatua mpya za kuleta umoja na maelewano chini ya uongozi wa waziri mkuu Bw. Abiy Ahmed zimekuwa na ufanisi, athari mbaya ya mivutano kati ya jamii tofauti imesababisha changamoto kwa uongozi mpya.

  Watu karibu milioni moja wamepoteza makazi na kuhitaji msaada wa dharura, haswa wakati wa majira ya mvua. Bw. Guterres amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua mara moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako