• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uingereza yatoa waraka wa makubaliano inayotaka katika kujitoa EU

  (GMT+08:00) 2018-07-13 18:49:34

  Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May imetoa waraka maalum unaoeleza kwa ufasaha makubaliano inayotaka na Umoja wa Ulaya (EU) baada ya nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja huo.

  Mkurugenzi mpya anayeshughulikia Brexit Dominic Raab amewasilisha mapendekezo ya waraka huo katika bunge la nchi hiyo. Bw. Raab alijibu maswali kadhaa ya wabunge kuhusiana na waraka huo, akisema kila kitu kimepangiliwa, lakini lengo lake ni kuona makubaliano ya kibiashara na nchi wanachama wa EU katika siku za baadaye.

  Vyombo vya habari nchini humo vinasema waraka huo umefanyiwa marekebisho ili kupunguza vikwazo kwa raia wa Ulaya wanaokwenda Uingereza baada ya nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako