• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yazungumzia ziara ya rais Xi Jinping nchini UAE, Senegal, Rwanda na Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-13 18:49:35

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya rais Xi Jinping nchini UAE, Senegal, Rwanda na Afrika Kusini.

    Naibu waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Kong Xuanyou amesema, ziara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na UAE, kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" katika sehemu ya Ghuba, na kuhimiza amani na utulivu wa Mashariki ya Kati. Pia itazidisha uaminifu wa kisiasa kati ya China na Afrika, kusaidiana kimaendeleo, kubadilishana mawazo, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika yenye uhusiano wa karibu zaidi. Amesema ziara hiyo itahimiza uhusiano kati ya China na nchi hizo, kuimarisha ushirikiano wa mshikamano kati ya China na nchi zinazoendelea za Asia na Afrika, na kukusanya maoni ya pamoja kwa ajili ya mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

    Akizungumza kwenye mkutano huo, Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Jun naye amesema, rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa 10 wa viongozi wa nchi za BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini. Amesema China inazingatia sana ushirikiano wa nchi za BRICS, na hii ni mara ya sita kwa rais Xi kuhudhuria mkutano wa BRICS. Umuhimu wa China katika kuhimiza na kuongoza ushirikiano wa BRICS umekubaliwa na pande mbalimbali. Ameongeza kuwa, kauli mbiu ya mkutano huo ni "nchi za BRICS katika bara la Afrika, kutafuta ongezeko shirikishi na ustawi wa pamoja katika mageuzi ya nne ya viwanda". China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini na pande nyingine kuhimiza mkutano huo kupata mafanikio na kutia nguvu mpya kwa ushirikiano wa BRICS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako