• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yataja watakaonufaika na msamaha wa kodi

    (GMT+08:00) 2018-07-13 19:03:04

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeainisha sifa za walipakodi watakaonufaika na msamaha wa madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu.

    TRA pia itatoa msamaha wa riba na adhabu ambayo utahusu kodi zote zinazotozwa kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na TRA isipokuwa ushuru wa forodha na mapato mengine yasiyo ya kodi kama kodi za kajengo na ada za matangazo.

    Hatua hiyo inakuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015.

    Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema jijini Dar es Salaam kuwa, serikali ilisikia kilio cha wafanyabiashara waliolalamikia kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu, na hivyo Bunge lilifanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sasa imeshaanza kufanyiwa kazi.

    Amesema, lengo kuu la msamaha huu ni kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi "Principal Tax" kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ili kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiyari na kwa wakati. Kamishna huyo alisema kuwa walipakodi watakaonufaika na utaratibu huo ni wale waliowasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo lakini pia wale ambao hawajawasilisha ritani za kodi na wana madeni ya kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako