• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATCL kupanua safari kote Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-07-13 19:03:47

    Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) linakusudia kuanzisha safari katika mikoa ya Tanga, Musoma, Shinyanga, Iringa na Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa.

    Ongezeko la vituo hivyo litatoa wigo kwa kila Mtanzania kunufaika na huduma zake hasa baada ya Serikali kuboresha huduma za usafiri wa anga.

    Mkurugenzi mtendaji wa ATCL Ladislaus Matindi amesema kwa sasa wanaendelea na utafiti kwenye viwanja ambavyo ndege zao zitaanza kufanya safari.

    Ameongezea kuwa wanakusudia pia kuongeza safari, badala ya mara moja ndege ziweze kwenda kwa siku mara mbili kwenye baadhi ya maeneo kama Dodoma.

    Akizungumzia ndege mpya, Boeing 787-8 Dreamliner, alisema itakuwa na marubani wanane ambao wote watakuwa ni Watanzania.

    Pia amewaomba Watanzania kuipokea ndege hiyo na kubainisha kuwa zipo mbili nyingine zitaingia mwezi Novemba.

    Licha ya Dreamliner iliyowasili Juni 8, ATCL inazo ndege tatu aina ya Bombardier zinazoendelea kutoa huduma.

    Kwa sasa ndege za shirika hilo zinatua Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Songea, Tabora, Kigoma, Bukoba, Mtwara pamoja na Visiwa vya Comoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako