• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yashambulia kambi ya jeshi la Syria jimboni Aleppo

    (GMT+08:00) 2018-07-16 09:49:26

    Israel imerusha makombora dhidi ya kambi ya kijeshi ya Syria jimboni Aleppo mapema jana na kusababisha uharibifu wa majengo.

    Shambulizi hilo limekuja baada ya Syria kutwaa udhibiti wa maeneo mengi ya jimbo ya Daraa, yakiwemo maeneo yaliyodhibitiwa na waasi karibu na eneo la milima ya Golan linalokaliwa na Israel.

    Habari zinasema, katika siku za karibuni, Israel imefanya mashambulizi mengi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Syria.

    Julai 11 mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria ulijibu shambulizi la ndege za Israel jimboni Quneitra, baadaye vyombo vya habari vya Syria vilitangaza kuwa ndege ya Israel ilitunguliwa kwenye shambulizi moja katikati ya Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako