• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari wa kulinda amani wa China watunukiwa "nishani ya amani" Darfur

    (GMT+08:00) 2018-07-16 10:10:30

    Askari 140 wa kikosi cha helikopta cha kulinda amani cha China wametunukiwa "nishani ya amani" huko Darfur, Sudan.

    Akizungumza kwenye hafla ya kuwatunuku nishani, mwakilishi maalum wa pamoja wa Tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur UNAMID Bw. Jeremiah Mambolo amesema kikosi cha kulinda amani cha China tawi la helikopta, kimefanya kazi nzuri katika kuleta amani na ukarabati pamoja na kutoa msaada wa kibinadamu katika eneo la Darfur.

    Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi hicho Bw. Chen Wenlong, hadi sasa kikosi cha helikopta cha kulinda amani cha China kimeruka kwa saa 800 kwa usalama, na kuwasafirisha watu elfu 5 na vifaa zaidi ya tani 200, na kwamba helikopta nne za kikosi hicho zimetekeleza majukumu katika maeneo 15 huko Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako