• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China umekua kwa asilimia 6.8 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-16 11:06:27

    Idara ya takwimu ya China imesema uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu umekua kwa asilimia 6.8, na kufikia thamani ya dola za kimarekani trilioni 6.27.

    Katika robo ya pili ya mwaka, ongezeko la uchumi wa China lilikuwa asilimia 6.7 ambalo ni chini kidogo kuliko ongezeko la robo ya kwanza, la asilimia 6.8.

    Msemaji wa Idara hiyo Bw. Mao Shengyong amesema katika kipindi hicho, uchumi wa China umeendelea vizuri na kuwa tulivu, ambapo mageuzi ya kimuundo yameimarishwa, misukumo mipya na ya jadi imeendelea kupokezana, na ubora na ufanisi wa uchumi vimeendelea kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako