• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa sherehe ya uzinduzi wa Chuo cha uongozi cha Nyerere

    (GMT+08:00) 2018-07-16 21:04:14

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi katika hafla ya uzinduzi wa Chuo cha uongozi cha Nyerere iliyofanyika leo nchini Tanzania.

    Katika barua yake, Rais Xi amesema, ujenzi wa chuo hicho uliofanywa kwa pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania, chama cha ANC cha Afrika Kusini, chama cha Liberation Front cha Msumbiji, chama cha ukombozi wa umma cha Angola, chama cha Labour cha Namibia pamoja na chama cha Zanu-PF cha Zimbabwe, ni hatua muhimu ya kuongeza ujenzi wa vyama hivyo na kuongeza uwezo wao wa utawala, ili kuchangia katika maendeleo ya nchi zao.

    Rais Xi pia amesisitiza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinapenda kutumia fursa hiyo kuhimiza hatua ya kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Afrika, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako