• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi ataka uhusiano wa karibu kati ya China na Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-07-17 07:28:07

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker, akitoa mwito wa kuwepo kwa uhusiano wa karibu zaidi kati ya China na Umoja wa Ulaya.

    Alipokutana na Bw. Tusk na Bw. Juncker jana hapa Beijing, rais Xi amesema China na Umoja wa Ulaya zinajenga amani ya dunia, kutoa mchango kwa maendeleo ya dunia na kulinda utaratibu wa kimataifa. Pia amesema China iko tayari kufanya kazi na Umoja wa Ulaya katika msingi wa usawa, haki, kuheshimiana na kunufaishana, kukuza zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya pande hizo mbili na ustawi wa watu.

    Habari nyingine zinasema China na Umoja wa Ulaya zimeahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kulinda utaratibu wa kimataifa uliojengwa kwenye msingi wa kanuni, kuhimiza utaratibu wa pande nyingi na kuunga mkono biashara huria.

    Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mkutano wa 20 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya ulioongozwa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, Bw. Tusk na Bw. Juncker.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako