• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump na Putin waridhika na mkutano wao, licha ya kutokuwa na matokeo halisi

    (GMT+08:00) 2018-07-17 09:14:21

    Rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Russia Vladmir Putin wameeleza kuridhishwa na mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana, licha ya kukiri kuwa bado kuna matatizo.

    Pamoja na kuwa mkutano huo umetajwa na Bw. Trump kuwa "siku ya kiujenzi" na Bw. Putin kuutaja kuwa ni " hatua muhimu ya kwanza" maswali kutoka kwa wanahabari kuhusu uingiliaji wa Russia kwenye uchaguzi wa Marekani, yalitawala mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mkutano wao.

    Rais Trump amesema alitumia muda mwingi kuongea na Rais Putin kuhusu tuhuma za uingiliaji wa Russia kwenye uchaguzi wa Marekani na Putin alikataa kuwa Russia iliingilia mambo ya ndani ya Marekani.

    Rais Putin amesema hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Russia iliingilia uchaguzi wa Marekani, na kusema kinachosemwa ni uvumi tu hakuna ushahidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako