• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi wa China akutana na katibu mkuu wa UNESCO Bibi Andrey Azoulay

    (GMT+08:00) 2018-07-17 09:21:07

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na katibu mkuu wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa mataifa Bibi Audrey Azoulay hapa Beijing.

    Akimkaribisha Bibi Azoulay kwa ziara yake ya kwanza nchini China, rais Xi amesema mustakbali na hatma ya watu wa dunia vimeunganishwa kwa karibu zaidi, na kusisitiza kuwa China inashikilia dhana ya kujenga "dunia yenye masikilizano", na kutoa wito kwa tamaduni mbalimbali kuheshimiana, kuwasiliana zaidi na kuelewana zaidi. Rais Xi amesema China inatilia maanani uhusiano kati yake na UNESO na inaunga mkono kithabiti nafasi muhimu ya UNESCO katika kusukuma mbele maendeleo ya dunia.

    Bibi Azoulay ameishukuru China kwa uungaji mkono kwa UNESCO, na pia amepongeza ushirikiano kati ya pande hizo mbili na kusifu msimamo wa China wa kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako