• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti waonesha mababu walitengeneza mikate kabla ya kuwa na ujuzi wa kilimo

    (GMT+08:00) 2018-07-17 09:22:29

    Wanasayansi wa Denmark na Uingereza wamegundua ushahidi wa kale zaidi wa mikate inayoaminika kutengenezwa miaka elfu nne kabla ya mababu wa binadamu kuwa na ujuzi wa kilimo. Utafiti uliotolewa jana umesema mabaki ya mikate iliyotengenezwa miaka 14,400 iliyopita yamegunduliwa kaskazini mashariki mwa Jordan, na kuonesha kuwa utengenezaji wa mikate kwa kutumia nafaka pori huenda uliwahamasisha wawindaji na waokotaji wa kale kulima mazao ya nafaka, na hivyo kuchangia mapinduzi ya kilimo kwenye zama za mawe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako