• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia 2018: Ufaransa na Croatia zapokewa kishujaa baada ya kila moja kuwasili nyumbani

    (GMT+08:00) 2018-07-17 10:17:43

    Timu mashujaa zilizofanikiwa kucheza mechi ya fainali ya kombe la dunia mwaka jana zimerejea nyumbani na kupokewa na mashabiki wao waliokusanyika kuwalaki katika miji mikuu ya nchi walikofikia.

    Mjini Paris, mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa walijipanga kando ya barabara kuanzia uwanja wa ndege ili kuwalaki wachezaji hao ambao baada ya kutua walisafiri kwa basi la wazi huku wakilionyesha kombe kutoka uwanja wa ndege hadi sehemu maarufu ya kufanyia mikusanyiko ya Champs Elysees ambako huko maelfu walijipanga kuwapokea.

    Tangu ufaransa watwae ubingwa wa dunia siku ya jumapili miji yote mikubwa ya nchi hiyo haikulala baada ya wananchi kuwa na sherehe zisizokuwa na kikomo wakiongozwa na serikali ya Rais Emmanuel Macron ambaye jana aliandaa hafla maalum katika ikulu kwa ajili ya timu hiyo.

    Lakini vivyo hivyo mjini Zagreb, washindi wa pili, timu ya taifa ya Croatia, ikiongozwa na mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia mwaka huu, Luka Modric, ililakiwa na mashabiki waliokuwa wamefurika kila kona ya mji huo.

    Na timu hiyo ikizunguka kwa basi la wazi kuanzia uwanja wa ndege hadi eneo maarufu kwa ajili ya mikusanyiko maalum la Bana Jelacica Square ambako huko maelfu walikusanyika kuwapokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako