• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yana uwezo wa kukabiliana na hali isiyotabirika ya uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2018-07-17 16:44:44

    Msemaji wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China amesema, katika nusu ya pili ya mwaka huu China ina imani na uwezo wa kutimiza malengo yaliyowekwa mwanzoni mwa mwaka huu, pia ina sera mwafaka za kukabiliana na hali isiyotabirika ya uchumi duniani.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa na serikali ya China, katika nusu ya kwanza mwaka huu, pato la taifa la China GDP liliongezeka kwa asilimia 6.8 likilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Msemaji wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Yan Pengcheng anaona hali hii imeonesha mustakabali mzuri na hali yenye utulivu iliyopo ndani ya uchumi wa China, na kuweka msingi imara katika kukabiliana na matishio mbalimbali. Katika nusu ya pili ya mwaka huu, uchumi wa China unatazamiwa kudumisha mwelekeo wa kupata maendeleo kwa hatua madhubuti. Anasema:

    "Muundo wa msukumo wa kuhimiza ongezeko la uchumi wa China umebadilika kutoka kutegemea zaidi uwekezaji na uuzaji wa bidhaa nje hadi kutegemea matumizi ya fedha, sekta ya huduma na mahitaji ya bidhaa kwenye soko la ndani. Katika miaka mitano iliyopita, idadi ya wateja katika soko la ndani imeongezeka kwa asilimia 80, na kufikia milioni 100. Msukumo huo umechangia theluthi moja ya ukuaji wa uchumi."

    Bw. Yan Pengcheng pia amesisitiza kuwa, China ina mfumo maalumu wa kisiasa, hali ambayo inasaidia China kufanya mambo mengi ambayo nchi nyingine zinashindwa kuyafanya. Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, China ilipata mafanikio katika kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo msukosuko wa fedha wa bara la Asia mwaka 1997, na msukosuko wa fedha wa kimataifa wa mwaka 2008 na kupata uzoefu mwingi, hali ambayo inaifanya ipate uwezo wa kukabiliana na changamoto kutokana na matishio mbalimbali. Anasema:

    "Tuna imani na uwezo wa kutosha kwa kutegemea ukuaji wenye hatua madhubuti wa uchumi wa China, kukabiliana kwa ufanisi na hali isiyotabarika ya uchumi wa dunia, ili kutimiza malengo yaliyowekwa mwanzoni mwa mwaka huu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako