• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asema urafiki kati ya China na Falme za Kiarabu ni wa kunufaishana

    (GMT+08:00) 2018-07-18 19:25:59

    Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kufanya ziara nchi za Falme za Kiarabu, UAE kuanzia kesho.

    Kabla ya ziara hiyo, rais Xi ameandika nakala kwenye gazeti la The National la nchi hiyo akisema, urafiki kati ya China na Falme za Kiarabu una historia ndefu, na ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, uzalishaji wa nishati, teknolojia mpya na za hali ya juu, mambo ya fedha, na mawasiliano ya kitamaduni zimepata mafanikio makubwa.

    Aidha rais Xi anatarajia kuwa, kupitia ziara hiyo, viongozi wa nchi hizo mbili wanaweza kuunda mipango ya siku za baadaye, kuzidisha ushirikiano, kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye hatma ya pamoja ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

    UAE ni kituo cha kwanza cha ziara hii ya kwanza ya rais Xi Jinping kwa mwaka huu, pia ni ziara ya kwanza katika nchi za Kiarabu tangu achaguliwe tena kuwa rais wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako