• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japani na Umoja wa Ulaya zashirikiana kufanya biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-07-18 19:51:25
     Umoja wa Ulaya na Japani leo zimesaini Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kichumi EPA, ambayo ni makubaliano makubwa zaidi ya biashara huria hadi sasa yanayotarajiwa kutekelezwa mwaka huu.

    Kama makubaliano hayo yakitelekezwa rasmi, eneo kubwa zaidi la uchumi duniani lenye watu milioni 600 na asilimia 30 ya pato la taifa la dunia nzima litazinduliwa.

    Ni kwa nini basi Japani inachagua wakati huu kusaini makubaliano ya EPA na Umoja Ulaya? Hatua hii inalingana na mpango uliowekwa na uhusiano wa kidiplomasia wa Japani, ambao pia ni mpango wake wa kushirikiana na Ulaya kupinga na kuondoa shinikizo la vikwazo vya kibiashara la Marekani.

    Kutafuta biashara na pande mbalimbali na biashara huria ni sera ya taifa iliyowekwa na Japani. Nchi hiyo inayochukua biashara kama msingi wa taifa, siku zote inatarajia kupata uongozi katika biashara na pande mbalimbali na kupata hadhi ya juu kwenye uhusiano na Marekani ili kuongoza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo.

    Kupitia makubaliano hayo, Japani inataka kutumia nguvu za nchi ndogo na za wastani kwenye sehemu hiyo kuimarisha nguvu yake ya kiuchumi na kisiasa. Hii ni hatua muhimu ya Japani kuonyesha heshima yake kwa Marekani, lakini kuondoa kihalisi ushawishi wa Marekani.

    Aidha, chini ya shinikizo la vikwazo vya kiuchumi vya Marekani na mazungumzo ya biashara za pande mbili, Japani inatafuta kupanua nafasi ya nje ya soko la uchumi na msingi wa uhusiano wa kiuchumi na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako