• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM asisitiza maendeleo na changamoto za kutimiza Ajenda ya mwaka 2030

    (GMT+08:00) 2018-07-19 09:26:59

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema wakati maendeleo yamepatikana kuelekea Ajenda ya mwaka 2030 kwenye maeneo kadhaa, bado kuna maeneo mengine ambayo yamepata maendeleo kidogo au hata kurudi nyuma.

    Akiongea kwenye mkutano wa kupitia maendeleo yaliyopatikana kuelekea Ajenda ya mwaka 2030, Bw. Guterres amesema maeneo yaliyopata maendeleo dhahiri ni pamoja na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto, kupanua elimu ya msingi na kuboresha upatikanaji wa umeme, lakini pia ametaja upungufu wa uwekezaji kwenye miundombinu endelevu, udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa migogoro na kukosekana kwa usawa, ukiukaji wa haki za binadamu na kuongezeka kwa misukosuko mikubwa ya kibinadamu, masuala ambayo amesema ni changamoto kubwa zinazozikabili juhudi za kutimiza ajenda ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako