• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya Marekani yataja matokeo ya mkutano kati ya Trump na Putin kuwa ni "mapendekezo madogo"

    (GMT+08:00) 2018-07-19 09:27:42

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bibi Heather Nauert amesema kuna matokeo matatu yaliyopatikana kwenye Mkutano kati ya rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Russia Vladimir Putin, ambayo yanaweza kuchukuliwa tu kama "mapendekezo madogo".

    Bibi Nauert amesema mapendekezo hayo yanahusisha kikosi kazi cha ngazi ya juu kinachoundwa na viongozi wa biashara wa nchi mbili, Baraza la wataalamu linaloshirikisha wataalamu wa sayansi ya siasa, wanadiplomasia na maofisa wa zamani wa jeshi, pamoja na mkutano kati ya mabaraza ya usalama ya taifa ya nchi hizo mbili utakaojadili "mikutano ifuatayo".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako