• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ulaya kuitoza faini ya euro bilioni 4.3 kampuni ya Google kutokana na ukiritimba wa Android

    (GMT+08:00) 2018-07-19 09:28:00

    Kamisheni ya Ulaya imesema inapanga kuitoza faini ya euro bilioni 4.3 kampuni ya tehama ya Google kutokana ukiritimba wa mfumo wake wa Android, kwa tuhuma za kukiuka kanuni za ushindani za Umoja wa Ulaya.

    Taarifa iliyotolewa na kamisheni hiyo inasema kuanzia mwaka 2011 Google imeweka vizuizi haramu dhidi ya watengenezaji wa zana zinazotumia mfumo wa Android na watoa huduma za mtandao kwa simu za mkononi, kwa lengo la kuimarisha hadhi yake ya utawala kwenye huduma za utafutaji kwenye Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako