• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zasifu ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-19 16:53:48

    Mkutano kuhusu mambo ya Afrika wa mazungumzo kati ya chama cha kikomunisti cha China CPC na viongozi wa vyama vya siasa vya dunia uliofungwa leo nchini Tanzania umepata mafanikio makubwa.

    Akihutubia sherehe ya ufungaji wa mkutano huo, naibu mkuu wa Idara ya mawasiliano na nje ya Chama cha CPC cha China Bw. Xu Lvping amesema, mkutano huo umefikia makubaliano kuhusu kufundishana kati ya vyama vya siasa vya China na Afrika, na kushirikiana kutafuta mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili. Katika siku hizo mbili, wawakilishi wa vyama 40 vya siasa kutoka China na nchi 40 za Afrika pamoja na baraza la Afrika, walijadiliana kuhusu vyama vya siasa vya China na Afrika kutafuta nadharia na njia ya maendeleo zinazolingana na hali ya nchi zao, na kutoa mipango kwa ajili ya kujenga uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika, na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili.

    Katibu mkuu wa chama tawala cha Jubilee cha Kenya Bw. Raphael Tuju amesema, mazungumzo hayo yametoa fursa nzuri kwa vyama vya pande hizo mbili kuwasiliana na kubadilishana uzoefu, anasema:

    "Mazungumzo hayo yametoa fursa nzuri ya kupeana uzoefu kati ya vyama vya siasa vya nchi mbalimbali za Afrika, ili kukuza maelewano kati ya vyama vya siasa vya Afrika na chama cha CPC cha China ambacho kina uzoefu mwingi wa utawala, na kupata uzoefu mzuri kuhusu kusaidia maendeleo ya nchi."

    Katibu wa mambo ya nje wa chama cha ukombozi wa umma cha Angola Bw. Juilao Mateus Paulo anaona kuwa, mazungumzo hayo yametoa utaratibu mzuri kwa mazungumzo kati ya China na Afrika akitumaini kuwa utaratibu huo utadumishwa. Anasema:

    "Utaratibu huo wa mazungumzo kati ya vyama vya siasa vya China na Afrika una kazi ya kusaidia. Natumai kuwa mwasiliano kama hayo yataweza kudumishwa, urafiki kati ya chama cha CPC cha China na vyama mbalimbali vya Afrika utaweza kuimarika, na kuleta matumaini mengi zaidi kwa maendeleo ya vyama vya siasa vya Afrika."

    Naibu katibu wa kudumu wa kwanza wa chama cha kikomunisti cha Afrika Kusini Bw. Solly Mapaila amesema, anaishukuru China kwa juhudi zake za kuunga mkono maendeleo ya Afrika. Akisema:

    "Mkutano huo umejumuisha watu wenye nadharia zinazofanana ambao wametoa mipango ya utatuzi wa kukabiliana na changamoto mbalimbali. China imeonesha umuhimu mkubwa wa kimkakati katika hatua hiyo. Naishukuru China kwa juhudi zake ilizofanya katika kuunga mkono maendeleo ya Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako