• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF lahimiza kundi la nchi 20 kutunga mpango wa kuboresha mfumo wa biashara ya pande nyingi duniani

    (GMT+08:00) 2018-07-19 19:31:36

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha IMF Bibi Christine Lagarde amehimiza watunga sera wa kundi la nchi 20 kutatua mgogoro wa kutoza ushuru kwa kulipizana kisasi, na kutunga mpango wa kuboresha mfumo wa utatuzi wa suala la biashara kwa njia ya pande nyingi .

    Bi Lagarde amesema, mwezi April shirika hilo lilitoa onyo kuhusu hasara zitakazoletwa na hatua za kujilinda kibiashara kwa uchumi wa dunia, kwa bahati mbaya onyo hilo limekuwa uhalisi. Takwimu mpya kutoka Ulaya na Asia zimeonesha kuwa mauzo ya bidhaa na imani ya nchi zinazouza magari ikiwemo Ujerumani imepungua.

    Mawaziri wa fedha na wakuu wa Benki Kuu za kundi la nchi 20 watakutana mjini Buenos Aires, na Bi Legarde amewahimiza kutumia fursa hiyo kumaliza hatua ya ushuru inayojiangamiza na kulipizana kisasi na kutunga mpango wa kuboresha mfumo wa biashara duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako