• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na UAE zashirikiana kujenga njia ya "Ukanda Mmoja na Nchi Moja" ya kunufaishana

  (GMT+08:00) 2018-07-19 20:11:46

  Rais Xi Jinping wa China leo atafanya ziara rasmi Falme za Kiarabu, UAE. Hii ni ziara ya kwanza katika nchi za kigeni tangu rais Xi achaguliwe tena kuwa rais wa China, na pia ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini humo katika miaka 30 iliyopita. Gloria Ngahyoma ametuandalia maelezo yafuatayo:

  Mwaka 2012, UAE na China zilianzisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati, na UAE ni nchi ya kwanza ya kiarabu ya ghuba iliyoanzisha uhusiano huo na China. Kufuatia mafanikio ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", China na kanda ya Mashariki ya Kati zimepata maendeleo katika miradi ya ushirikiano ya mafuta na gesi asilia.

  Mbali na hayo, UAE na China zimezidisha ushirikiano katika sekta za ujenzi wa miundombinu, mawasiliano ya simu, fedha na utamaduni. UAE imepongeza sana pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa na China, hivyo ziara ya rais Xi itainua ushirikiano wa karibu kati ya pande hizo mbili katika kiwango cha juu zaidi.

  Ushirikiano kati ya China na UAE pia unaweza kuhimiza ushirikiano wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kati ya China na Mashariki ya Kati. Kwenye pendekezo hilo, Mashariki ya Kati ipo kwenye kituo cha katikati na mawasiliano, na pia ni eneo la asili la ushirikiano. Hivi sasa China ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi 9 za kiarabu, na nchi hizo pia ni eneo kubwa zaidi linalotoa mafuta asili kwa China, ambazo pia ni mwenzi wa saba kwa ukubwa wa biashara na soko muhimu la nje la miradi na uwekezaji kwa China.

  Kwa nchi za Mashariki ya Kati, pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ni fursa ya kihistoria ya maendeleo isiyoweza kuikosa. Pande hizo mbili zimeshirikiana mara nyingi, huku malengo ya maendeleo ya pande mbili yakiendana na sekta za ushirikiana zikisaidiana, hivyo mustakabali wa kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni mkubwa sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako