• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fursa za uwekezaji Dodoma

    (GMT+08:00) 2018-07-19 20:33:07

    Usimamizi wa mkoa wa Dodoma ukishirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wameainisha maeneo 65 yenye fursa ya uwekezaji katika halmashauri saba na jiji la Dodoma.

    Dk Binilith Mahenge mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema maeneo yaliyoainishwa ni ya fursa za kuwekeza miradi mikubwa ya kijamii na ya kiuchumi katika halmashauri na jiji zima.

    Amesema, maeneo hayo ni 20 yanayofaa kwa ajili ya kuwekeza rasilimali za majengo na nyingine. Pia walibainisha maeneo 14 ya uwekezaji katika kilimo, maeneo 10 yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa taasisi za mafunzo mbalimbali na maeneo saba yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

    Maeneo sita yanayofaa kwa stendi za mabasi, wakati maeneo mengine sita yanafaa kwa ajili ya uegeshaji malori na maeneo mawili yanafaa kwa ajili ya miradi ya ufugaji," amesema.

    Dk Mahenge amesema, mkoa huo unafaa kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo hayo kutokana na ardhi, hali ya hewa na uoto wa asili rafiki kwa watakaotaka kuwekeza katika mkoa huo.

    Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema wamejiandaa kukaribisha wawekezaji kwa kupima viwanja vya kutosha kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako