• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cricket: Kenya wanyakua kombe la michuano kusaka teketi ya kombe la Dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:17:36
    Timu ya taifa ya Kenya ya Kriketi imenyakua kombe la kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia mnamo mwaka 2020 nchini Australia. Ni michezo ilizozikutanisha nchi za Afrika mashariki ilioyochezewa uwanja wa kimataifa wa Gahanga, Kigali.

    Kenya imeshinda kwa alama 10, Uganda ikifuatia kwa alama 8, Tanzania wao wameambulia nafasi ya tatu kwa kupata alama 6.

    Timu ya Rwanda ambayo ndio walikuwa wenyeji haikushinda mechi yoyote kati ya 6 walizozicheza na haina hata alama moja.

    Kwa matokeo hayo, Kenya na Ugandawamekata tiketi ya kucheza dhidi ya timu za kanda nyingine za Afrika kwa ajili ya kuchagua watakaoshiriki kombe la Dunia 2020 nchini Australia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako