• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema lengo la mwaka 2020 la dunia katika mapambano dhidi ya UKIMWI huenda halitatimizwa

    (GMT+08:00) 2018-07-20 17:11:03

    Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa UNAIDS limesema, huenda lengo la kudhibiti maambukizi mapya ya UKIMWI na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kuwa chini ya laki 5 mwaka 2020 halitafikiwa.

    Ripoti iliyotolewa na Shirika hilo imesema, ingawa mafanikio makubwa yamepatikana katika udhibiti na kinga ya ugonjwa wa UKIMWI, lakini idadi ya maambukizi mapya ya VVU na watu wanaofariki kutokana na UKIMWI bado haijapungua kwa kasi.

    Ripoti hiyo imesema, juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo zilizofanywa na jamii ya kimataifa ziko katika hali ya hatari, hivi sasa kasi ya maendeleo ya mapambano dhidi ya UKIMWI haiendani na lengo lililowekwa. Hivyo ili kutumiza lengo hilo muhimu, nchi mbalimbali zinatakiwa kuchukua hatua mara moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako