• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Paul Kagame wa Rwanda aonesha matumaini yake kwa ziara ya rais Xi Jinping wa China

  (GMT+08:00) 2018-07-20 17:24:13

  Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara ya kihistoria nchini Rwanda hivi karibuni, rais Paul Kagame wa Rwanda amepokea mahojiano ya pamoja ya vyombo vya habari vya China mjini Kigali, akieleza matarajio yake kwa ziara hiyo ya rais Xi , kupongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kusifu nadharia ya kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja".

  Kutokana na mwaliko wa rais Paul Kagame, rais Xi Jinping wa China atafanya ziara ya kitaifa nchini Rwanda kuanzia tarehe 22 hadi 23, na hii itakuwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa China kuizuru Rwanda, vilevile ni kujibu ziara ya iliyofanywa na rais Kagame wa Rwanda mwezi Machi mwaka 2017 nchini China. Rais Kagame anaonesha furaha kubwa na matumaini makubwa juu ya ziara hiyo ya rais Xi. Anasema:

  "Uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, na China na Rwanda una historia ndefu, nafurahi sana kuona rais Xi amepokea mwaliko wangu kuizuru Rwanda. Baada ya ziara hiyo, urafiki kati ya China na Afrika, na China na Rwanda utazidi kuimarishwa, natumai kuwa mawasiliano kati ya pande zetu mbili yanaweza kuimarishwa."

  Rais Kagame anaona ziara ya rais Xi Jinping wa China itakuwa na umuhimu mkubwa akisema:

  "Ziara ya rais Xi Jinping kwa Rwanda ina umuhimu mkubwa hata kwa bara la Afrika. Atahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS nchini Afrika Kusini, na utakuwa ushirikiano wa pande mbili na wa pande nyingi utakaojumuisha nchi za Afrika na nchi nyingine, na watu wa nchi hizo wanaweza kutafuta kwa pamoja maendeleo na kunufaishwa kwa pamoja."

  Rais Kagame wa Rwanda anasifu sana wazo la rais Xi kuhusu kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja". Anasema:

  "La muhimu zaidi ni kuwa wazo hilo la rais Xi linaziunganisha sehemu mbalimbali duniani kutafuta maendeleo ya pamoja. Kupitia ujenzi wa 'Ukanda mmoja, Njia moja', mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi mbalimbali yataimarishwa na kuzinufaisha nchi zote duniani."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako