• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la kiraia kati ya China na Afrika kufanyika huko Chengdu

    (GMT+08:00) 2018-07-20 18:51:50

    Shirikisho la mawasiliano ya kimataifa ya mashirika ya kiraia la China na serikali ya mkoa wa Sichuan litafanya Baraza la tano la kiraia kati ya China na Afrika huko Chengdu kuanzia tarehe 23 hadi 24 mwezi huu, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya hatma ya pamoja kati ya China na Afrika kwa upande wa kiraia.

    Kauli mbiu ya baraza hilo ni Kukusanya nguvu za kiraia na kuhimiza uaminifu na urafiki kati ya China na Afrika. Zaidi ya wajumbe 200 wa mashirika 140 ya kiraia kutoka nchi zaidi ya 30 watashiriki kwenye baraza hilo.

    Baraza hilo litatangaza miradi 30 ya ushirikiano wa kiraia kati ya China na Afrika itakayotekelezwa katika miaka mitatu ijayo, ambayo ni pamoja na ushirikiano na uchangishaji fedha kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu, ujenzi wa uwezo na mawasiliano ya wataalamu, maendeleo ya jamii, mawasiliano ya utamaduni na jamii, na mawasiliano ya kiraia kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako