• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China nchini Rwanda asema ziara ya rais Xi nchini Rwanda itahimiza uhusiano kati nchi hizo mbili 

  (GMT+08:00) 2018-07-21 10:05:40

  Kutokana na mwaliko wa rais Paul Kagame wa Rwanda, rais Xi Jinping wa China ataanza ziara yake rasmi nchini Rwanda tarehe 22 hadi tarehe 23 Julai. Kabla ya ziara hiyo, balozi wa China nchini Rwanda Bw. Rao Hongwei aliwaambia wanahabari wa nchi hizo mbili kuwa, ziara hiyo ya rais Xi Jinping itahimiza uhusiano kati ya China na Rwanda uingie kwenye zama mpya, na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

  Akisisitiza umuhimu wa ziara hiyo, Balozi Rao amesema hii ni mara ya kwanza kwa rais wa China kufanya ziara nchini Rwanda katika historia, sekta mbalimbali nchini Rwanda zina matarajio makubwa kwa ziara hiyo, ambapo rais Xi Jinping na mwenzake rais Paul Kagame watafanya majadiliano kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na hali iliyopo ya kanda husika, ili kutoa mwelekeo na kupanga mustakabali wa uhusiano huo.

  Balozi Rao amesema China inaiunga mkono Rwanda katika juhudi za kukuza uchumi, kulinda usalama na utulivu. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 hadi 90 ya barabara na madaraja nchini Rwanda zimejengwa na kampuni za China. Ziara ya rais Xi sio tu itaweka msingi thabiti wa kisiasa, bali pia itaimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na kuhimiza kwa kiasi kikubwa katika kujenga uhusiano mwema kati ya China na Rwanda na hatma ya pamoja kati ya China na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako