• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Senegal asema pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja litawanufaisha watu wa Afrika na China

    (GMT+08:00) 2018-07-21 11:10:33
    Rais wa Senegal asema pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja litawanufaisha watu wa Afrika na China

    Kutokana na mwaliko wa rais Macky Sall wa Senegal, rais Xi Jinping wa China anafanya ziara rasmi nchini Senegal tarehe 21 hadi tarehe 22 Julai. Kabla ya ziara hiyo, rais Sall aliwaambia wanahabari wa China kuwa, ziara ya rais Xi Jinping ina umuhimu wa kihistoria kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili na mustakabali wake.

    Rais Sall amesema anakaribisha China kushiriki kwenye "Mpango wa ufufuaji wa Senegal", serikali za nchi hizo mbili zitasaini makubaliano mbalimbali, na kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi kupitia miradi ambayo China inatoa misaada au mikopo, na kujenga uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya ulio na wenye uvumbuzi kati yao.

    Rais Sall amesema kuna mengi ya kujifunza kutoka China katika kuendeleza, kwani China ilichukua miaka 40 kufanya uchumi wake uwe wa kisasa, na kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi, Afrika inahitaji mwenzi kama huyu ili kujipatia maendeleo.

    Mbali na hayo, rais Sall pia amesifu pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, linalojengwa katika uhusiano wa kushirikiana, kunufaishana, na kufanya biashara kwa usawa, kurahisisha mawasiliano ya kimataifa, na litaunganisha watu wa nchi mbalimbali, haswa wa Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako