• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fikra ya Xi Jinping kuhusu kufanya mageuzi na kufungua mlango yatoa uelekezaji mpya kwa China katika Zama Mpya

    (GMT+08:00) 2018-07-21 12:12:00

    Kitabu cha "Utafiti wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango" kimechapishwa hivi karibuni, hiki ni kitabu maalumu cha kufafanua Fikra ya Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango na Maendeleo ya China katika Zama mpya, kitabu hiki kimefuatiliwa na kusifiwa na watu wengi wa sekta husika.

    Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, miaka 40 imepita tangu sera ya Deng Xiaoping ya kufungua mlango wa China itekelezwe nchini China mwaka 1978, hivi sasa mambo ya mageuzi ya China yanaendelezwa kwa kina na kwa pande zote, Fikra ya Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango imetoa uelekezaji muhimu zaidi wa kinadharia kwa ajili ya China kupiga hatua mbele ya ukuaji wake, walisema, "Kihalisi, Xi Jinping amekuwa msanifu mkuu wa China katika Zama Mpya".

    "Kitabu cha Utafiti wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango" ni kitabu cha kwanza cha nadharia ambacho kimefanya uchambuzi na ufafanuzi kwa pande zote kuhusu Fikra ya Xi Jinping inayohusu mageuzi na kufungua mlango.

    Wataalamu na wasomi wanaohusika wa China wameona kuwa, Fikra ya Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango ni sehemu muhimu ya Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China katika Zama Mpya. Kuchapishwa kwa kitabu hiki kimetoa silaha ya nadharia yenye nguvu zaidi kwa ajili ya kufanya majumuisho juu ya Fikra ya Xi Jinping kuhusu mageuzi na kufungua mlango, na kupiga hatua mbele ijayo ya China kufanya mageuzi na kufungua mlango.

    Tangu Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike, Xi Jinping akiwa katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama amepanga na kuhimiza moja kwa moja mpango kabambe wa kimkakati wa kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote. Xi Jinping amesema, kufanya mageuzi na kufungua mlango ni "hatua moja muhimu sana ya kuamua mustakabali wa China katika zama tulizonazo".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako