• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa makala kwenye gazeti la New Times la Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-07-21 16:32:02

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala kwenye gazeti la New Times la Rwanda yaitwayo "Urafiki kati ya China na Rwanda ni mkubwa zaidi".

    Kwenye makala hiyo, rais Xi Jinping amesema, ingawa China na Rwanda ziko mbali sana, ukubwa wa ardhi, utaratibu na utamaduni ni tofauti, lakini watu wa nchi hizo mbili wana urafiki mkubwa wa jadi. Tangu mwaka 1971 nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, China na Rwanda zinashikilia urafiki wa udhati na kutendeana kwa usawa. Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Rwanda umeendelezwa kwa kasi, ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa.

    Kwa sasa, Rwanda inafanya juhudi kutimiza mpango wa maendeleo ya mwaka 2020, na China inajitahidi kutimiza malengo ya "Miaka 100 ya Chama na Miaka 100 ya Taifa". Maendeleo ya ushirikiano kati ya CHina na Rwanda yanakabili fursa ya kihistoria.

    Rais Xi Jinping amesema anatumai kwa kupitia ziara yake hiyo kutia nguvu mpya kwa urafiki wa jadi na ushirikiano wa pande mbalimbali kati ya China na Rwanda, kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufikia kiwango kipya, na kupata mafanikio mapya, ili kunufaisha wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako