• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo kikuu cha radio na telivisheni cha taifa cha China na kituo cha telivisheni cha taifa cha Senegal zasaini makubaliano ya kurusha tamthilia ya China

  (GMT+08:00) 2018-07-21 17:19:22

  Sherehe ya uzinduzi wa mpango wa kuonesha filamu na tamthilia za China kwenye eneo la lugha ya kiufaransa barani Afrika imefanyika tarehe 19 mwezi Julai huko Dakar nchini Senegal.

  Mkuu wa kituo cha Ulaya ya Magharibi cha CRI Bw. Gao Shijun kwa niaba ya kituo kikuu cha radio na telivisheni cha taifa cha China pamoja na mkuu wa kituo cha radio na telivisheni cha taifa cha Senegal Bw. Racine Talla wamesaini makubaliano kuhusu kuzindua program ya tamthilia za China kwenye kituo cha telivisheni cha taifa cha Senegal.

  Kutokana na makubaliano hayo, program hiyo itaonesha tamthilia za China zilizotafsiriwa na kuwekwa sauti za kiufaransa na CRI.

  Mjumbe maalum wa ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China Bw. Zhang Yanbin alitoa pongezi kuwa mpango huo una umuhimu mkubwa wakati wa ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Senegal. Amesema kuwa tamthilia ina umaalumu wa kuwasiliana hisia ya watu na kutimiza mawasiliano ya kiutamaduni ambao ni njia muhimu ya kuzidisha uelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili, akitumai tamthilia hizo zitakaribishwa na marafiki wa Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako