• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hamas na Israel wakubaliana kusimamisha mapigano

    (GMT+08:00) 2018-07-21 18:49:49

    Kundi la Hamas jana limetangaza kuwa limefikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel baada ya matukio kadhaa ya migogoro kwenye mpaka wa Gaza.

    Msemaji wa Hamas Bw. Fawzi Barhoum amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi zilizoongozwa na Misri pamoja na Umoja wa Mataifa.

    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, pande zote zinapaswa kufuata makubaliano hayo yaliyofikiwa usiku wa manane siku ya ijumaa, na waache kuhasimiana.

    Wakati huo huo, jana wapalestiana wanne wameuawa na wengine 210 wakijeruhiwa kutokana na mapigano ya kutisha yaliyotokea kati ya Israel na Hamas, yakidaiwa kuwa makubwa zaidi tangu vurugu zianze kwenye mpaka huo mwaka 2014.

    Inaelezwa kuwa mapigano hayo yalizuka baada ya mwanajeshi mmoja wa Israel kuuawa wakati wa shughuli za kusimamia usalama kwenye eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza siku hiyo ya jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako