• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari nchini Somalia waua mtu mmoja na kujeruhi watatu

    (GMT+08:00) 2018-07-21 19:32:01

    Polisi nchini Somalia, wamesema mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

    Mlipuko huo umetokea katika eneo lililo karibu na kaburi la mwanajeshi wa zamani ambaye hata hivyo hakutambulika, baada ya bomu lililokuwa limetegwa chini ya gari kulipuka.

    Waliojeruhiwa ni mwanaume mmoja na wanawake wawili na wote wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

    Aidha, kutokana na mlipuko huo, polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini sababu na wahusika wa mlipuko huo, kwa kuwa mpaka sasa hakuna kundi lolote lililojitangaza kuhusika.

    Mlipuko huu umetokea ikiwa ni wiki moja baada ya kundi la kigaidi la al-Shabab kutekeleza mlipuko mwingine kwenye kituo cha ukaguzi wa magari kilichopo karibu na ikulu, na kuua watu wawili kikiacha wengine wengi wakijeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako